Watoto walindwe dhidi ya mitandao ya internet:ITU

11 Februari 2014

Muungano wa kimataifa wa mawasiliano ITU umeungana na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa, asasi za kiraia na serikali pamoja na makampuni ya teknolojia katika kuadhimisha siku ya mtandao wa internet salama duniani leo tarehe 11 February inayoangazia mkakati wa kieleimu kukuza usalama wa matumizi ya internet kwa watoto na vijana.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni kujenga mtandao bora wa internet pamoja , ITU inasongesha juhudi za kuwalinda watoto katika mitandao kwa kutoa muongozo kw awatoto, wazazi, watunga sera pamoja na makampuni ya teknolojia katika lugha sita rasmi za Umoja wa Mataifa.

ITU inasema utafiti unaonyesha kuwa karibu nusu ya watoto katika nchi za Ulaya wanaweza kupata mitandaoni katika vumba vyao na robo yao ambao wana umri kati aya miaka 12 hadi 15 wanamiliki vifaa maaluma ambavyo vina mtandao, vinavyofahamika kwa jina la tablet.

Utafiti huo pia unaonyesha kuwa matumizi ya simu za kisasa zenye mtandao wa internet kutuma na kupokea picha za kawaida na video yamekuwa huku mbinu za kiusalama kwa watoto ili kuwalinda hazijakua zikilinganishwa na ukuaji wa teknolojia hizo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud