Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanahabari wanawake katika radio watakiwa kuzingatia maadili na kushinda vishawishi.

Wanahabari wanawake katika radio watakiwa kuzingatia maadili na kushinda vishawishi.

Katika kuelekea siku ya radio duniani February 13, wanawake walioko katika tasnia ya habari hususani katika radio wametakiwa kuzingatia maadili ya kazi ili kukabiliana na kujiepusha na vishawishi na kutekeleza majukumu yao.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Salim Chiro wa radio washirika Pwani Fm iliyoko Mombasa, mwanahabari mkongwe nchini Kenya Zakia Muhamedi ambaye amkuwa katika tasnia hiyo kwa zaidi ya miaka 30 ameema licha ya vishawishi ambavyo wanawake wanaofanya kazi katika radio wanakutana navyo ipo fursa ya kukabiliana navyo ikiwa watajiamini.

(SAUTI ZAKIA)

Mahojiano kwa urefu na mwanahabari huyo nguli nchini Kenya yatapatikana katika ukurasa wetu.