Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

AU na UM wasaini Mkataba wa kupinga ukatili wa kingono sehemu za zenye vita.

AU na UM wasaini Mkataba wa kupinga ukatili wa kingono sehemu za zenye vita.

Mkataba wa ushirikiano kati ya muungano wa Afrika Au,  na Umoja wa Mataifa, UM kuhusu kukinga na kuzuia ukatili wa kingono katika sehemu za vita barani Afrika umesainiwa mnamo Janury January 31 ikiwa ni siku ya mwisho ya mkutano wa muungano wa Afrika au.

Mkataba huo utatumika kama mkakati mkuu kwa ajili ya ushirikiano wa kina katika maeneo muhimu kama vile kupambana na ukwepaji sheria kwa watekekelezaji wa vitendo hivyo, uwezeshaji na mafunzo kwa walinda amani na wanausalama pamoja na kuimarisha sera za mataifa, katiba na sheria zaifanyazo kazi katika maeneo ambayo ukatili wa kingono vitani unatendeka.

Kadhalika makataba huo unasisistiza umuhimu wa huduma kwa manusura wa ukatili wa kingono , uwezeshaji wa wanawake na wasichana  na kukabiliana na unyanyapaa kwa manusura.

Kwa upande wake mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kingono kwenye maneneo yenye mizozo Zainab Hawa Bangura aliyeatia saini mkataba huo kwa niaba ya Umoja huo amesifu hatu hiyo na kuwapongeza viongozi kwa kujitoa kutekeleza makataba huo. Amesisistiza umuhimu wa juhudi za  serikali kukabiliana na vitendo hivyo wakati na baada ya vita.

Aliyesaini kwa niaba ya Muungano wa Afrika ni kamishna wa amani na usalama ndani ya AU Balozi Smaïl Chergui.