Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yajivunia mafanikio ya uwezeshaji Radio za kijamii Tanzania hususan kwenye maendeleo ya kijinsia

UNESCO yajivunia mafanikio ya uwezeshaji Radio za kijamii Tanzania hususan kwenye maendeleo ya kijinsia

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Teknolojia, UNESCO linajivunia harakati zake za kuleta usawa wa kijinsia kupitia mafunzo yake ya kuziwezesha radio hususan zile za kijamii kwenye nchi zinazoendelea.Miongoni mwao ni zile za nchini Tanzania ambapo katika mahojiano na Assumpta Massoi wa Idhaa hii,  Mratibu wa Mawasiliano wa shirika hilo kwa Radio za Kijamii Al Amin Yusuph anaanza kwa kueleza kile walichofanya na kuleta mabadiliko chanya kwa watendaji wa Radio hizo na jamii zinazozizunguka.

(Mahojiano)