Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kutatua mizozo ya kikabila Sudan wafanyika Darfur

Mkutano wa kutatua mizozo ya kikabila Sudan wafanyika Darfur

Ujumbe wa pamoja wa muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa Darfur Sudan (UNAMID) kwa kushirikiana na taasisi ya utafiti wa amani ya chuo kikuuu cha Khartoum mwishoni mwa juma  wamefungua kongamano la siku mbili kuhusu uelewa wa vita vya  kikabila mjini Darfur.

Kongamano hilo linahudhuriwa na maprofesa, wasomi na wanaharakati mbalimbali  linajikita katika mambo muhimu kuhusu vyanzo na madhara ya vita vya kikabila huko Darfur pamoja na upatanishi.

Wahudhuriaji wa mkutano huu wanatarajiwa kutoa mapendekezo ya vitendo juu ya namaa kutatua  ghasia ambapo katika ufunguzi wa mkutano huo siku ya jumapili mwakilishi wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa Darfur Mohamed Ibn Chambas amesema mwaka jana umeshuhudia mapigano ya kikabila yasiyotarajiwa na yasiyokuwa ya kawaida jimbioni Darfur nchini Sudani.