Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

China yatoa taarifa kuhusu ongezeko la watu waliokumbwa na virusi A(H7N9)

China yatoa taarifa kuhusu ongezeko la watu waliokumbwa na virusi A(H7N9)

Serikali ya China imeendelea kutoa taarifa zinazofahamisha kuwepo kwa ongezeko la watu wanaokumbwa na virusi vya A(H7N9) ambavyo tayari vimesabisha kifo cha mtu mmoja nchini humu tangu kuzuka kwake.

 
Kulingana na maelezo yaliyotolewa kwa shirika la afya ulimwenguni WHO, kumekuwa na ongezeko la watu waliokumbwa na virusi hivyo waliofikia nane baada ya kubainika wengine kufuatia uchunguzi wa kimaabara.
 
Kati ya nane hao, sita ni wanaume wenye umri kati ya miaka 5 hadi 73. Watu watano wanatajwa kuwa katika hali mbaya zaidi.
 
Kutokana na hali hiyo serikali ya China imesema kuwa inaendelea kuchukua hatua za haraka kukabiliana na kitisho hicho ikiwemo kuyaweka katika uangalizi maalumu maeneo yaliyokumbwa na virusi hivyo.