Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwezeshaji wa Radio za kijamii Tanzania umezaa matunda: UNESCO

Uwezeshaji wa Radio za kijamii Tanzania umezaa matunda: UNESCO

Katika kuelekea siku ya Radio duniani, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Teknolojia, UNESCO nchini Tanzania limesema jitihada zake za kuwezesha Radio za kijamii nchini humo kupitia usaidizi wa kuandaa sera za jinsia na vipindi umekuwa chachu katika utendaji wa vituo hivyo na kwa jamii zinazozunguka.

Mratibu wa mawasiliano wa UNESCO nchini Tanzania kuhusu Radio za Kijamii, Al Amin Yusuph akizungumza na Idhaa hii ametolea mfano Radio Sengerema mkoani Mwanza ambayo amesema kitengo cha Radio kinaongozwa na wanawake na ushiriki wa wanawake kwenye uandishi na utangazaji umeongezeka.

(Sauti Al Amin)
 
Hata hivyo amesema bado kuna changamoto ikiwemo baadhi ya sera za kitaifa kutojumuisha Radio za kijamii na hata mfumo dume kukwamisha wanawake kusikiliza vipindi vya kuwawezesha kupata habari za maendeleo.

Mahojiano kamili  na Afisa huyo wa UNESCO Tanzania kuhusu uwezeshaji wa Radio za kijamii Tanzania, yanapatikana kwenye tovuti yetu.