Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa usawa unaweza kuepukika: ILO

Ukosefu wa usawa unaweza kuepukika: ILO

Chapisho jipya la shirika la kazi duniani, ILO linasema kuwa tofauti kati ya matajiri na maskini ina uhusiano kiasi na mabadiliko ya teknolojia lakini ni matokeo ya sera za kiuchumi na kitaasisi zilizotangulia mdororo wa kiuchumi na kuchochewa  zaidi na janga la kijamii. Hata hivyo ILO inasema tofauti hizo zinaweza kukwepeka, Assumpta Massoi na taarifa zaidi.

 (Taarifa Assumpta)

Chapisho hilo la leo liitwalo ukuaji unaochagizwa na mishahara linatupia lawama kidogo tu mbadiliko ya teknolojia katika mwelekeo wa usawa duniani na mzigo mkuu unaelekezwa kwa sera za kitaifa zilizokuwepo kwa kipindi cha miaka 30 iliyopita ambazo limesema zimesababisha mgao wa kipato wa misingi ya kibepari.  Matahalani imetaja kile kijilikanaxho kama ujira wa kazi kuwa kilianza kuporomoka miaka ya 1980 kwenye nchi tajiri kama vile Marekani na Japan na mwelekeo huo umeanza kwenye nchi zinazoibukia kama vile China. ILO imesema mgao wa ujira umependelea zaidi matajiri dhidi ya maskini kwa miaka 20 iliyopita na hata kongamano la kimataifa la uchumi la Davos lilibaini hivyo.

Chapisho hilo linasema hali hiyo inaweza kupatiwa suluhu na jibu ni kuangaliwa upya kwa sera ili ziweke ukuaji wenye uwiano zaidi jambo ambalo ILO inasema lahitaji uratibu wa sera kimataifa.