Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yasafirisha wahamiaji wa Rwanda waliofurushwa Tanzania

IOM yasafirisha wahamiaji wa Rwanda waliofurushwa Tanzania

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limetoa msaada wa dharura kwa zaidi ya raia wa Rwanda 15,000 waliorudishwa kutoka Tanzania kwa kipindi cha miezi sita iliyopita.

Mkuu wa IOM nchini Rwanda Catherine Northing amesema inakadiriwa kuwa wanyarwanda ambao hawana vibali vya kuishi wamefurushwa licha ya kwamba idadi ya wahamiaji hao wanaowasili mipakani ni ndogo kwa sasa.

Wakimbizi hao walilazimika kurejea makwao kufuatia agizo la serikali ya Tanzania mwaka jana la kuondoka kwa wahamiaji wote katika mkoa wa Kagera kwa hiari au kuondolewa na vikosi vya ulinzi.

IOM Inasema hadi kufikia Januari 21 mwaka huu wahamiaji zaidi ya elfu 14 theluthi yao wakiwa wanawake na wengi wao wakiwa wajawazito, wamewasili katika mpaka kati ya Tanzania na Rwanda.