Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vifo vitokanavyo na surua vimepungua kwa kiwango kikubwa zaidi: WHO

Vifo vitokanavyo na surua vimepungua kwa kiwango kikubwa zaidi: WHO

Idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa wa surua kila mwaka imeshuka kwa asilimia 77 kutoka mwaka 2002 hadi mwaka 2012, na hivyo kuzuia zaidi ya vifo milioni 13, limesema Shirika la Afya Duniani, WHO.

WHO imetangaza hayo wakati wa uzinduzi wa ripoti yake ya makadirio ya vifo vitokanavyo na surua.

Ugonjwa wa surua unaambukiza mno, na dalili zake huwa ni homa, upele na dalili kama za mafua. WHO imesema kushuka kwa idadi hiyo ya vifo kumetokana chanjo za kimataifa na zile za kawaida zitolewazo kwa watoto.

WHO imetoa chanjo kwa takriban watoto milioni 145 katika kampeni ya chanjo ya halaiki mnamo mwaka 2012. Licha ya mafanikio hayo, ugonjwa wa surua bado ni tatizo barani Afrika, mashariki ya bahari ya Mediterenia na maeneo ya Ulaya