Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa kuchunguza athari za matangazo ya biashara kwa haki za utamaduni

Umoja wa Mataifa kuchunguza athari za matangazo ya biashara kwa haki za utamaduni

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za utamaduni, Farida Shaheed, amezindua utafiti mpya katika athari za matangazo ya biashara kwenye haki za tamaduni za watu. Utafiti huo utazingatia hasa athari za matangazo hayo kwenye utofauti wa tamaduni na haki za binadamu.

Ataangazia pia athari za ufadhili wa kibiashara kwenye haki miliki za usomi na sanaa, pamoja na vitu vinavyopatikana katika majumba ya makumbusho na masuala mengine.

Ripoti ya utafiti huo itazingatiwa kwenye Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo mwezi Oktoba mwaka huu. Bi Shaheed amesema tatizo moja ambalo matangazo ya biashara yanaweza kuleta kwenye utofauti wa kitamaduni ni pale yanapoathiri haki ya watu kuchagua jinsi wanavyotaka kuishi.