Skip to main content

Utapia mlo huenda ukakatili maisha ya watoto 50,000 Mali:UM

Utapia mlo huenda ukakatili maisha ya watoto 50,000 Mali:UM

Mashirika ya misaada nchiniMaliyameelezea hofu yake juu ya kiwango kikubwa cha utapiamlo nchiniMalina kuonya kuwa watoto wapatao 50,000 wanaweza kufariki dunia mwaka huu. Taarifa ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi

(TAARIFA YA ASSUMPTA MASSOI)

Mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Mali David Gressely amesema anasema ufadhili wa haraka unahitajika ili kupeleka bidhaa za lishe katika maeneo yaliyoathirika zaidi na utapia mlo.

Amesema ingawa hali ya usalamaMaliimeimarika kiasi familia takribani milioni 3.3 zinakabikliwa upungufu wa chakula kutokana na athari za mgogoro wa mwaka 2012 na 2013, lakini pia kutokana na mavuno hafifu mwaka jana.

Ameongeza kuwa raia 168,000 waMalibado wanishikamawakimbizi katika nchi jirani huku wengi wao wakisita kurejea nyumbani kutokana na hofu ya usalama.

 “Tunatarajia zaidi ya watoto 400,000 wataathirika na utapia mlo mwaka 2014. Zaidi ya wengine 100,000  wanauwezokano mkubwa kupata ule uliokithiri ambao huambatana na idadi kubwa ya vifo.Hivyo ni muhimu kuhakikisha kuhakikisha msaada wa lishe unapatikana kwa mwaka mzima wa 2014. Baadhi ya mikoa yenye utajiri wa kilimo nchini Mali ina idadi kubwa ya kiwango cha utapia mlo . inakanganya kwa kiasi lakini ndio ukweli , hivyo ni muhimu kutojikita tuu maeneo ya Kaskazini. Kuna haja ya msaada wa kibinadamu Kaskazini mwa nchi , sawa na ilivyo haja ya kushughulikia mahitaji ya nchi nzima Mali ambako tatizo la utapia mlo na usalama mdogo wa chakula sinasalia kuwa suala linalotia hofu kwa raia wa Mali.”

Umoja wa mataifa umetoa ombi la dola milioni 569 ili kukabiliana na mahitaji ya kibinadamu nchiniMalikwa mwaka huu wa 2014.