Shambulio dhidi ya wizara ya mambo ya nje ya Iraq lalaaniwa na UM:

5 Februari 2014

Shambulio dhidi ya ofisi za wizara ya mambo ya nje yaIraqambalo limekatili maisha ya watu na kujeruhi wengine limelaaniwa vikali na Umoja wa Mataifa.

Imearifiwa kwamba mabomu mawili yaliyokuwa yametegwa kwenye magari yameripuka nje ya wizara ya mambo ya nje mjiniBaghdadsiku ya Jumatano.

Machafuko ya kidini yameshika kasi mwaka jana nchiniIraq. Kwa mujibu wa msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Farhan Haq , mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa nchini Iraq Nickolay Mladenov, ametoa wito wa kuwepo na umoja na mshikamano kufuatia mashambulizi hayo.

Amesema walioandaa mashambulizi hayo lazima walaaniwe vikali na viongozi wote wa kisiasa, kidini na kijamii nchiniIraq.

Pia ameongeza kuwa viongozi wa kisiasa ni lazima waonyeshe umoja wa kitaifa katika kukabiliana na vitishokamahivyo na kuungana dhidi ya ugaidi.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter