Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Radio imekuwa chombo cha thamani kwa wanawake wakulima huko Sengerema, Tanzania

Radio imekuwa chombo cha thamani kwa wanawake wakulima huko Sengerema, Tanzania

Katika kuelekea siku ya Radio duniani tarehe 13 mwezi huu, tathmini mbali mbali zimeendelea kufanyika kubaini uwezeshaji wa jinsia kupitia Radio. Mathalani, makundi ya wanawake yamenufaika vipi kupitia Radio? Wawe ni wasikilizaji au ni watendaji.. Mwenzetu Pauline Mpiwa wa Radio Washirika Sengerema FM iliyoko Mwanza nchini Tanzania aliamua kuangazia wanawake wakulima kuona wao Radio ina manufaa gani kwao, na hivyo basi ungana naye kwenye makala hii.