Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hispania yahimizwa kuziamini vyombo vyake vya maamuzi

Hispania yahimizwa kuziamini vyombo vyake vya maamuzi

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa Pablo de Greiff ameiambia Hispania kwamba haipaswi kuwa na wasiwasi juu ya vyombo vyake vya utoaji maamuzi na kwamba haina haja ya kuhairisha mchakato wake unaolenga kuwatendea haki waathirika wa vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu vilivyofanywa na dikteta Franco wakati kulipuzuka machafuko ya kiraia. Joseph Msami na maelezo zaidi.

(Taarifa ya Msami).

Mtaalamu huyo juu ya haki amesema kuwa Hispania ni taifa lililopevuka kwa demokrasia hivyo halipaswi kuwa na wasiwasi wowote kwani vyombo vyake vya maamuzi vimekomaa na vinaweza kutenda haki bila vikwazo vyovyote.

Akizungumza mwisho mwa ziara yake, de Greiff alitaja hatua muhimu za maridhiano ambazo zinapaswa kutekelezwa wakati huu ili waathirika wa machafuko hayo wanafikiwa na fidia.

Alitaka pia kuanzishwa kwa uchunguzi maalumu ili hukakisha kwamba yale yaliyojitokeza miaka ya nyuma hajatirudii tena na kwamba serikali inawajibika kutafuta njia za haki kuwafidia waathirika.

Akiwa nchini humo mtaalamu huyo alitembelea maeneo kadhaa ya kumbukumbu ikiwemo Valle de los, jela iliyojulikana Canal  na makaburi ya halaiki.