Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Takribani miaka 20 baada ya mkutano wa Beijing, wanawake bado wanakumbwa na madhila: Ban

Takribani miaka 20 baada ya mkutano wa Beijing, wanawake bado wanakumbwa na madhila: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema mwaka 2015 ni mwaka muhimu sana ambao pamoja na kuwa ukomo wa malengo ya maendeleo ya milenia, pia ni miaka 20 tangu mkutano wa kimataifa wa wanawake wa Beijing ulioweka mwelekeo wa hatua za usawa wa kijinsia.

Bwana Ban amesema hayo baada ya tukio maalum la kupiga picha hii leo kwenye Makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, na Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa Marekani Bi. Hillay Clinton na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja huo linalohusika na wanawake UN-Women Phumzile Mlambo-Ngcuka.

Katibu Mkuu amesema katika miaka 20 ya Mkutano wa Beijing, licha ya mafanikio yaliyopatikana bado kuna changamoto na kwamba suala la usawa wa jinsia ni mojawapo ya vipaumbele vyake.

"Tumekuwa na maendeleo makubwa tangu mwaka 1995. lakini hado wanawake wengi wanakumbwa na ubaguzi na ukatili. Tunapaswa kubadili fikra hizo. Nimejitolea kwa dhati kushirikiana nawe na ninakutegemea sana kwa uongozi wake na ushirikiano wako na Umoja wa Mataifa kwenye hili.”

Bwana Ban amesema baadayel leo anakwenda huko Urusi kwenye ufunguzi wa mashindano ya olimpiki ya majira ya baridi mjini Sochi ambako atatumia fursa hiyo kuchochea nafasi ya michezo katika kuunganisha watu bila kujali jinsia, kabila na umri.