Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vifo 490 vimesababishwa na mapigano ya kikabila nchini Kenya 2013:OCHA

Vifo 490 vimesababishwa na mapigano ya kikabila nchini Kenya 2013:OCHA

Takriban watu 490 wamepoteza maishayaokatika machafuko ya kikabila Kaskazini mwa Kenya mwaka 2013 imesema ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA.

Shirika hilo linasema zaidi ya watu wengine 1,200 walijeruhiwa na wengine zaidi ya 47,000 kulazimika kuzikimbia nyumba zao. Limeongeza kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la mapigani kwa mwezi wa Desemba.

Kwa mujibu wa OCHA mapigano hayo ya kikabila yametokana na ushindani dhidi ya uwakilishi wa kisiasa, ardhi na rasilimali. Maeneo yaliyoathirika saana na machafuko hayo ni vitongoji vya Moyale, Mandera  naTana River.