Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Barizi yarejea kwenye Ufukwe wa Lido Somalia

Barizi yarejea kwenye Ufukwe wa Lido Somalia

Nchini Somalia kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab kiliendesha vitendo vya vitisho na kubadili mfumo wa maisha ya watu. Mathalani watu waliopenda kubarizi kwenye maeneo ya fukwe kwenye mji mkuu Mogadishu walihofia mashambulizi yaliyokuwa yakifanywa na kundi hilo eneo hilo.

Hata hivyo juhudi za Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika zimeleta nuru kwenye maeneo ya aina hiyo na sasa amani imereja na watu wanaweza kupumzika kama inavyoelezea makala hii inayoletwa kwako na Grace Kaneiya.