Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kila anayeumwa ana haki ya kupata dawa za kupunguza maumivu zilizoidhinishwa: INCB

Kila anayeumwa ana haki ya kupata dawa za kupunguza maumivu zilizoidhinishwa: INCB

Rais wa Bodi ya Kimataifa ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya, Raymond Yans, amesisitiza umuhimu wa mikataba ya kimataifa ya udhibiti wa madawa hayo katika kuhakikisha kuwa dawa zilizoidhinishwa zipo na zinatumiwa vizuri katika kutuliza maumivu na kuwaondolea wagonjwa machungu.

Akizungumza kwenye kikao cha 109 cha bodi hiyo, Bwana Yans amesema watu wote wana haki za kupata dawa ambazo zimedhibitiwa kimataifa na kuruhusiwa katika kutuliza maumivu, akizingatia kuwa viwango vya saratani vimeongezeka, hususan katika nchi zinazoendelea.

Ameongeza kuwa upatikanaji wa dawa za kupunguza maumivu zitokanazo na afyuni haupo sawa kwa wote.