Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Saratani bado ni changamoto kubaini mapema ndio tiba: WHO

Saratani bado ni changamoto kubaini mapema ndio tiba: WHO

Leo ni siku ya saratani duniani ambapo Shirika la afya ulimwenguni WHO linasema kuwa ugonjwa huo kwa sasa ni chanzo kikuu cha vifo ukiwa umesababisha vifo vya watu Milioni Nane Nukta Mbili mwaka 2012. Saratani zinazoongoza ni ile ya mapafu, tumbo, ini, utumbo mpana na ile ya titi. Ujumbe wa mwaka huu ni vunja ukimya na ondokana na fikra potofu juu ya saratani ambapo watu huogopa kujitokeza na hivyo kuchelewa kugundulika ili kupata tiba. Nchini Tanzania katika hospitali ya rufaa ya Bugando hata hivyo Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake Dokta Nandi Ng’warida anasema mkoani humo saratani inayoongoza ni ile ya shingo ya kizazi.

(Sauti ya Dkt, Nandi)

Habari njema ni kwamba Shirika la kimataifa la nguvu za atomiki, IAEA linasema teknolojia ya nyuklia ikiwemo minururisho ni muhimu katika kubaini saratani mapema pamoja na tiba.

Mathalani imesema katika miongo minne imeweza kutoa usaidizi wa tiba ya aina hiyo kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Vietnam ambako kunatokoea asilimia 70 ya vifo vyote vya saratani.