Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jamii zaidi zaendelea kuchana na mila potofu ya ukeketaji:UM

Jamii zaidi zaendelea kuchana na mila potofu ya ukeketaji:UM

Tarehe Sita Februari ndio siku husika ambapo mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la idadi ya watu UNFPA na lile la watoto, UNICEF yamesema harakati hizo zimezaa matunda lakini bado mila hiyo inatekelezwa na hivyo yanatekeleza programu ya kuona jamii zaidi zinaachana nayo.

Yamesema kampeni inayohusisha wadau wote ni muhimu kwani baadhi ya nchi Misri ukeketaji unafanywa na wahudumu wa tiba na hivyo kuhalalisha kitendo hicho dhalili. Laura Gehrke ni afisa wa UNFPA.

(Sauti ya Laura)

Katika miaka ya karibuni sheria imepitishwa katika nchi tatu, usimamizi wa sheria umeendelezwa na huduma zimeimarishwa na kupitia vyombo vya habari, masuala kuhusu ukeketaji yamekuwa yakitangazwa. Iwapo hatutafanya lolote watoto wapatao Milioni 86 duniani kote watatumbukia kwenye mila hiyo ifikapo mwaka 2030.”

Umoja wa Mataifa unasema kuwa mikakati ya misingi ya haki za binadamu ni muhimu ili  kuhakikisha watoto wa kike na familia zao ambao wanaondokana na mila hiyo hawapotezi matarajio yao ya ndoa au kutengwa na jamii zao.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa wasichana Milioni Tatu wenye umri wa chini ya miaka 15 hukeketwa kila mwaka na hivyo kuathiri tu si afya zao bali pia maendeleo yao kijamii.