Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kobler awasihi waandamanaji DRC kutumia njia za amani kuwasilisha madai yao

Kobler awasihi waandamanaji DRC kutumia njia za amani kuwasilisha madai yao

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC Martin Kobler ametaka waandamanaji kutumia njia za amani kuelezea matakwa yao.

Ametoa kauil hiyo baada ya ripoti ya kwamba watu hao walishambulia kwa mawe magari kadhaa ya Umoja wa mataifa kwenye mji wa Bunia na kusababisha majeruhi wanne akiwemo mlinda amani mmoja.

Bwana Kobler ambaye pia ni mkuu wa ofisi ya Umoja wa MAtaifa ya kuweka utulivu DRC, MONUSCO amesema shambulio kama hilo la leo dhidi ya raia na watendaji wa Umoja huo halikubaliki kwa misingi yoyote ile.

Kwa mujibu wa MONUSCO polisi wa DRC waliingilia kati tukiohilona kuidhibiti kwa minajili ya ushirikiano wao na polisi wa Umoja wa Mataifa.