Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNAMA alaani shambulio dhidi ya wanakampeni za uchaguzi

Mkuu wa UNAMA alaani shambulio dhidi ya wanakampeni za uchaguzi

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, Ján Kubiš, ameshutumu vikali shambulio lililosababisha mauaji ya watendaji wawili wa timu ya kampeni ya mgombea wa Urais nchini humo Dokta Abdullah Abdullah.

Katika taarifa yake Kubiš amesema watu hao walipiga risasi na watu wenye silaha wasiojulikana siku ya Jumamosi kwenye mji wa Heart. Kubiš ambaye ni mkuu wa ofisi za Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNAMA ametaka mamlaka nchini Afghanistan kuwasaka wahusika na kuwafikisha mbele ya sheria.

Ametaka mamlaka za usalama nchini humo kuchukua hadhari ya hali ya juu kwenye wiki zijazo za kuelekea uchaguzi tarehe Tano mwezi Aprili mwaka huu.