Wajumbe wa Baraza la Usalama wafanya ziara nchini Mali

3 Februari 2014

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wako ziarani nchiniMalikutathmini hali halisi baada ya mzozo uliosababisha madhara makubwa ya kiuchumi, kisiasa na kijamii.  Taarifa zaidi na Assumpta Massoi

(Taarifa ya Assumpta)

Wajumbe hao pamoja na kutembelea kambi ya kikosi cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuleta utulivu nchiniMali, MINUSMA mjiniBamakowamekuwa na mazungumzo na Rais Ibrahim Boubacar Keïta. Wakiwa Mopti, takribani kilometa 600 kutokaBamakowalijulishwa changamoto za usalama kutoka kwa vikundi vya kijihadi na tishio la kiuchumi kutokana na mzozo pamoja na kuendelea kuwasili kwa wakimbizi wa ndani kutoka Kaskazini. Mwakilishi wa kudumu wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Gerard Araud ni miongoni mwa waliopo kwenye msafara.

(Balozi Araud)

“Tunataka utulivu nchini Mali, na huo tunafahamu vyema utapatikana kwa mashauriano kati ya serikali na vikundi vyenye silaha. Mali imetekeleza mengi..uchaguzi umefanyika vizuri  na taasisi za kikatiba. Na sasa inatakiwa kukamilisha mashauriano na vikundi vyeney silaha na tu mefika kushuhudia na serikali wamefikia wapi kwenye hilo na jinsi gani tunaweza kuwasaidia.”