OCHA kutoa ombi la dola bilioni 1.3 kwa ajili ya Sudan Kusini

3 Februari 2014

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA itatoa ombi la dola bilioni 1.3 katika siku zijazo kwa ajili ya watu walioathirika na machafuko nchini Sudan Kusini. Kwa mujibu wa mratibu wa misada ya kibinadamu Sudan Kusini Toby Lazer , fedha hizo zitatumika kununua vifaa visivyokuwa chakula kwa maelfu ya watu walioathirika na vita. Ameongeza kuwa Umoja wa mataifa unafanya kazi pamoja na wizara ya inayohusika na masuala ya kibinadamu ili kuratibu ombi hilo.

(SAUTI YA TOBY LANZER)

Watu wenye mahitaji hususani ni ya chakula na mamilioni ya wengine watahitaji misaada ya aina nyingine ikiwemo mablanketi, maji na vyoo. Kwa hiyo ni muhimu kukumbuka kwamba kuna sehemu tatu, wakimbizi walioko katika kituo cha Umoja wa Mataifa ni sehemu tu, wakimbizi wa ndani walioko kote nchini ni sehemu nyingine na  jumla ya watu wote walio na mahitaji sudan Kusini  ni ya juu takribani  mtu mmoja kwa kila watu watatu.

Lanzer amesema watu wapatao milioni 3.7 wanahitaji msaada wa haraka wa chakula kutokana na vita Sudan Kusini.