Ladsous kufuatialia utekelezaji wa makubaliano Sudan Kusini

31 Januari 2014

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Hervé Ladsous Jumapili hii atakuwa na ziara nchini Sudan Kusini ambapo pamoja an mambo mengine atazungumza na viongozi waandamizi wa serikali na upinzani kuhusu utekelezaji wa makubailano ya kusitisha mapigano yaliyotiwa saini mwezi huu huko Ethiopia.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amewaambia waandishi wa habari kuwa Bwana Ladsous atatembelea pia ofisi za ujumbe wa Umoja wa Mataifa UNMISS ambako atakuwa na mazungumzo na watendaji na kuwashukuru kwa vile wanavyojitolea kulinda raia licha ya changamoto za usalama.

UNMISS inasema hadi sasa inahifadhi zaidi ya raia 85,000 kwenye vituo vyake nchini kote huku ikiwa imetibu zaidi ya wagonjwa Elfu Moja kwenye kituo chake cha afya huko Malakal. Pamoja na kutoa tiba, imeweza kutoa huduma za uzazi ambapo watoto 28 wamezaliwa kwenye kituo hicho tangu mwezi Disemba.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter