Baraza la Usalama laongeza muda wa kundi azimio la udhibiti wa silaha DRC

30 Januari 2014

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limeptisha azimio la kuongeza muda wa azimio la udhibiti wa silaha katika DRC, ambalo ni azimio namba 1807 la mwaka 2008 hadi tarehe 1 Februrari, 2015.

Azimio hilo pia linaongeza muda wa vikwazo vya kifedha na usafiri dhidi ya watu au makundi yanayolikiuka, vikiwalenga viongozi wa kisiasa na wa makundi ya kigeni ya kijeshi yanayoendesha shughuli zao katika DRC au kuyasaidia makundi yenye silaha.

Pia azimio hilo linawalenga watu wanaozuia usambazaji wa misaada ya kibinadamu katika DRC, pamoja na wale wanaoongoza mauaji, ubakaji, utekaji nyara, kulazimu watu kuhama na kufanya mashambulizi dhidi ya taasisi za umma kama shule na hospitali.

Baraza hilo pia limemwomba Katibu Mkuu kuongeza muda wa kundi la wataalam wanaochunguza hali katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC hadi Februari 1, mwaka 2015. Mwakilishi wa kudumu wa DRC kwenye Umoja wa Mataifa, IgnaceGata Mavita wa Lufuta amezungumza kuhusu wataalam hao katika mkutano na waandishi wa habari…

“Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inakubali ripoti ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa. Ripoti hii inatoa taarifa muhimu kuhusu hali ya nchi yangu hususan ile inayohusu wapiganaji wa zamani wa M23 ambao kama mnavyojua walifurushwa na jeshi letu na sasa hivi wako wakimbizi Uganda na Rwanda. Ripoti ya wataalamu inasema kuwa wafuasi wao wako katika harakati za kujikusanya upya,  na hata kabla ya kwenda ukimbizini kwenye nchi hizo walipata usaidizi kutoka Rwanda. Na tumetoka kuonyesha wasiwasi wetu mbele ya Baraza la Usalama, kwa sababu iwapo tunasaka amani siyo tu DRC bali eneo lote, haipaswi nchi jirani ambayo imetia saini makubaliano ya amani, ulinzi na ushirikiano kando inatoa msaada kwa makundi hayo, na hiyo ni kinyume na makubaliano ya amani. Hilo ndilo tulilosema.”

 Baraza hilo limelaani vikali makundi yote yenye silaha yanayoendesha shughuli zake katika eneo la mashariki mwa DRC na ukiukwaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu na za haki za binadamu, na kutaka makundi ya FDLR, ADF na LRA na yale ya Mayi Mayi kukomesha mara moja aina zote za machafuko na vitendo vyao vya vinavyoharibu utulivu.