Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ALMA yatoa tuzo kwa nchi Saba za Afrika kwa kudhibiti Malaria

ALMA yatoa tuzo kwa nchi Saba za Afrika kwa kudhibiti Malaria

Mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Muungano wa Afrika umeanza leo hukoAddis Ababa, Ethiopia ambapo pamoja na mambo mengine wametangaza nchiSabazilizoshinda tuzo ya kudhibiti Malaria. Taarifa zaidi na Joseph Msami.

(Taarifa ya Joseph)

Ni Kamishna wa masuala ya kijamii ndani ya Muungano wa Afrika Dokta Mustapha Sidiki Kaloko akitangazaMalawikuwa miongoni mwa nchi Saba zilizoibuka kidedea kwenye vita dhidi ya Malaria na kushinda tuzo hiyo iliyotolewa na ushirikiano wa viongozi wa Afrika dhidi ya Malaria,ALMAkwa mwaka huu wa 2014.

Mmoja baada ya mwingine alijitokeza kupokea tuzo akiwemo pia Rais Hifikepunye Pohamba waNamibiana Paul Kagame waRwanda. Nchi zingine niCape Verde,Madagascar,Swazilandna Sao Tome naPrincipe.  Kamishna Kaloko akafafanua sababu za ushindi.

(Sauti ya Dkt. Kaloko)

"Idadi kubwa ya nchi hizi zimefikia lengo la kimataifa la kupunguza Malaria kwa angalau asilimia 75 tangu mwaka 2000. Walikuwa pia na kiwango kikubwa cha udhibiti wa mazalia ya mbu na hivyo kusababisha kupungua kwa wagonjwa kutoka Milioni 1.6 mwaka 2000 hadi zaidi ya Laki Tatu na Nusu mwaka 2012. Na wengine walifanya vizuri sana kushawishi fedha kutoka taasisi ya global Fund na PMI ili kupunguza Malaria.”

 Katika hatua nyingine mkutano wa AU umezindua rasmi mwaka 2014,kama mwaka wa kilimo na uhakika wa chakula barani Afrika.