ICTR yatoa mwongozo wa kukabiliana na uhalifu wa kingono baada ya vita

30 Januari 2014

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Uhalifu wa Kimbari wa Rwanda, ICTR, leo imetoa mwongozo wa kina unaoeleza njia bora za kuandaa mashtaka dhidi ya uhalifu wa kingono katika maeneo yanayoibuka kutoka kwa migogoro. Joshua Mmali na taarifa kamili

(Taarifa ya Joshua)

Mwongozo huo unatokana na uzoefu wa takriban miaka 20 ya kuendesha mashtaka dhidi ya washukiwa wa uhalifu wa kingono ulotendeka wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

Wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, ubakaji na aina nyingine za ukatili wa kingono vilitumiwa kama njia ya kueneza mauaji, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Mwongozo wa ICTR unatoa vidokezi vya vinavyoweza kutumiwa na waendesha mashtaka wengine wa kimataifa na kitaifa ambao wamepewa majukumu ya kuchugnguza na kufanya mashtaka dhidi ya uhalifu wa aina hiyo. Hatua kwa hatua, ofisi ya ICTR inaeleza ilichojifunza kutokana na ilichokifanya na kile ambacho kingefanywa.