Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

M.A.C, Rihanna na UNAIDS waungana kuwafikia vijana milioni 2 wanaohitaji dawa za HIV

M.A.C, Rihanna na UNAIDS waungana kuwafikia vijana milioni 2 wanaohitaji dawa za HIV

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuighulika na masuala ya ukimwi UNAIDS limetangaza Alhamisi upanuzi wa mradi wake wa tiba ya HIV wa mwaka 2015 baada ya kupewa dola milioni mbili na fuko la kampuni ya kimataifa ya vipodozi M.A.C .

Fedha hizo zimepatikana baada ya mauazo ya rangi ya kupuka mdomo maarufu kala lip stick aina ya VIVA GLAM na Lipglas, kwa msaada mkuvbwa wa mwanamuziki wa kimataifa Rihana ambaye anatumia umaarufu wake kuchagiza mauzo ya urembo huo na pia kuelimisha kuhusu maambukizi ya HIV.

Kwa fedha hizo UNAID itapanua wigo wa mradi wa 2015 kimataifa, kikanda na katika ngazi ta taifa ikihamasisha uwepo wa sera na mipango ya kuongezxa upimaji na tiba kwa vijana duniani kote.

Rais wa bidhaa za MAC John Demsey amesema wateja, rasilimali za UNAID na kumtumia Rihanna kuunga mkono kampeni hii kunasaidia kuokoa maisha ya maelfu watu.

Inakadiriwa kuwa duniani kote vigori, barubaru na vijana milioni 5.4 wanaishi na virusi vya HIV na milioni 1.8 ndio wanaopata dawa huku mamilioni hawajuikamawameambukizwa virusi.

Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa UNAIDS Michel Sidibe  kila siku takribani vigori, barubaru na vijana 2100 wanapata maambukizi mapya ambao ni sawa na asilimi 39 ya maambukizi yote mapya. Mradi wa tiba 2015 una lengo la kufikia watu wazima na vijana milioni 15 ifikapo mwaka 2015.