Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sitarajii mafanikio "makubwa" kwenye awamu ya kwanza ya mazungumzo ya Syria: Brahimi

Sitarajii mafanikio "makubwa" kwenye awamu ya kwanza ya mazungumzo ya Syria: Brahimi

Mjumbe maalum wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa nchi za kiarabu kwenye mzozo wa Syria Lakhdar Brahimi amesema hana matumaini makubwa sana na matokeo ya awamu ya kwanza ya mazungumzo kati ya pande mbili kinzani kwenye mzozo huo.

Brahimi amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari baada ya awamu ya leo ya mashauriano ya ana kwa ana na ujumbe wa serikali na ule wa upinzani, pande ambazo amesema hii ni mara ya kwanza kukutana tangu kuanza kwa mzozo miaka mitatu iliyopita na licha ya kukutana bado tofauti ni kubwa.

(Sauti ya Brahimi)

“Niseme wazi tu sikutarajia kupata mafanikio makubwa. Ninafurahi kwamba bado tunazungumza, lakini mambo yanafunguka taratibu. Ijumaa tutaahirisha na tutajadili kile ambacho tutafanya baada ya kukutana tena. Natumai kuwa awamu ya pili ya mazungumzo itakuwa imepangika vizuri na itakuwa fanisi kuliko awamu ya kwanza.”

Bwana Brahimi amesema Ijumaa watakubaliana tarehe ya kukutana tena penginepo baada ya wiki moja.