Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marta, Gattuso , Vieri kushiriki mchezo wa kihisani kukabili njaa

Marta, Gattuso , Vieri kushiriki mchezo wa kihisani kukabili njaa

Wachezaji kadhaa wa soko wakiwemo Marta Vieira da Silva, Genaro Gattuso, Christian Vieri, na Phillip Cocu ni miongoni mwa waliothibitisha kuungana na wachezaji nyota Ronaldo na Zinédine Zidane katika mchezo uliolenga kukabiliana na njaa

Mechi hiyo iliyopangwa kufanyika baadaye mwaka huu itakuwa ni ya 11 katika jitihada za shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP kukabiliana na majanga ya njaa katika maeneo mbalimbali duniani.

Fedha zitakazopatikana katika mchezo huo zitatumika kuwakirimu mamia ya raia wa Ufilipino walioathiriwa na kimbunga kilichoikumba nchini hiyo mwishoni mwa mwaka jana.

 Wachezaji wengine watakakuwepo kwenye mechi hiyo ni pamoja Steve McManaman Robert Pires, Makélélé,Jens Lehmann na Freddie Ljunberg