UN-Women na Taasisi ya Mara zaungana kusaidia wajasiriamali wanawake Afrika

29 Januari 2014

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN Women kwa ushirikiano na Taasisi ya Mara wametangaza ubia wenye lengo la kuwawezesha na kuwatia moyo wajasiriamali wanawake barani Afrika.

Ubia huo umetangazwa rasmi hukoAddis Ababa,Ethiopiakando mwa harakati za maandalizi ya kikao cha wakuu wa Muungano wa Afrika, AU kinachoanza kesho.

Taarifa ya pamoja ya taasisi hizo imesema kupitia ubia huo wajasiriamali hao watapatiwa mafunzo na stadi za kuwawezesha kukidhi sifa za wajasiriamali wa karne ya sasa barani humo.

Mathalani wanawake watakutana na wajasiriamali waliobobea na kujifunza kutoka kwao na hata kupatiwa ushauri.

Akizungumzia ubia huo Mkurugenzi Mtendaji wa UN-Women Phumzile Mlambo-Ngcuka amesema kuwawezesha wanawake kiuchumi ni njia muhimu ya kutokomeza umaskini na kusongesha mbele usawa wa kijinsia.

Amesema shirikalakelimefurahisanakuungana na Taasisi ya Mara kufikia lengohilokwani wanawake wanapowezeshwa, mafanikioyaohuvuka mipaka.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter