Mawaziri wa AU waweka ajenda za kikao cha viongozi, watambua makubaliano Sudan Kusini

29 Januari 2014

Wakati Mkutano wa wakuu wa nchi za Muungano wa Afrika, AU ukitarajiwa kuanza kesho Alhamisi hukoAddis Ababa,Ethiopia, kikao cha mawaziri wa nchi hizo wametambua makubaliano ya hivi karibuni ya pande zinazokinzana Sudan Kusini na kupendekeza utekelezaji ili yaweze kunufaisha wananchi. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Mwakilishi wa Kudumu waTanzaniakwenye Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi amesema hayo katika mahojiano na idhaa hii kutokaAddis AbabaEthiopiaanakohudhuria kikao cha mawaziri hao kinachoandaa ajenda kwa ajili ya mkutano wa viongozi wa AU unaoanza Alhamisi mjini humo.

(Sauti ya Balozi)

Suala jingine ni suala la viongozi waKenyakushtakiwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC ambapo Balozi Manongi amesema pamoja na kuwa itakuwepo, mawaziri nao wamerejelea msimamo wa AU…

(Sauti ya Balozi)

Ajenda nyingine ni mustakhabali wa Afrika katika kujiondoa na utegemezi wa utekelezaji wa shughuli zake za maendeleo ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Afrika wa maendeleo 2063 pamoja na uwakilishi wa Afrika kwenye uandaaji wa ajenda ya maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015.