Watoto wakimbizi wa Sudan Kusini wapatiwa chanjo ya surua Uganda

29 Januari 2014

Takribani watoto Elfu Saba katika kambi ya wakimbizi Nyumanzi na ile ya muda ya Dzaipi nchini Uganda wamepatiwa chanjo dhidi ya Surua kufuatia kuzuka kwa maradhi  hayo wiki iliyopita.

Kampeni hii inatekelezwa na  mashirika ya Umoja wa Mataifa ya UNICEF na UNHCR kwa ushirikiano na serikali ya Uganda na inakabiliwa na changamoto ya fedha kutokana na kuendelea kumiminika kwa wakimbizi kutoka Sudan Kusini. Ripoti kamili na John Kibego wa redio washirika ya Spice FM, Uganda.

 (TARIFA YA JOHN KIBEGO)

Kampeni hii iliyoanza siku ya Jumapili baada ya visa vitatu vya surua kugunduliwa katika jamii ya wakimbizi wilayani Adjumani, inawalenga watoto wote kati ya umri wa miezi sita na miaka 15. Kando ya watoto  hao 6915 wa wakimbizi, watoto wengine 1492 raia wa Uganda katika jamii jirani za kambi hizo nao wamechanjwa.

Godfrey Manda Afisa Msaidizi wa afia wilayani Adjumani anasema, zisingelikuwa changamoto za kifedha, kampeni hii ingelifanyike kote wilayani kwa sababu wakimbizi wengi wamejichanganya na na wanainchi vijijini na mijii.

 (Sauti ya Godfrey Manda)

 "Dawa tulizonazo hazitoshi, rasilimali hazitoshi ndiyo maana tunafanya kampeni hii katika kambi ambao zimeathiriwa peke. Naona tunafanya hakitoshi kwa sababu tuna wakimbizi katika sehemu mbali mabali kote wilayani na hata mjini hapa.”

Hata hivyo Manda amesema, baada ya kuwapa chanjo watoto katika kambi hizo mbili, wataenda katika kambi nyingine tatu kwa sababu wanajua, Wasudani Kusini wengi walikimbia makwao kabla ya kupata huduma za afia silahili kwa watoto wao.

Kampeni kama hii ya chanjo dhidi ya surua, inaendelea katika kambi za wakimbizi wilayani Arua Muihso.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter