Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akutana na Fidel Castro: Wajadili Syria, Sudan Kusini na mengineyo

Ban akutana na Fidel Castro: Wajadili Syria, Sudan Kusini na mengineyo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ambaye yuko ziarani nchini Cubaamekuwa na mazungumzo na Rais wa zamani wa nchi hiyo Fidel Castro Ruz mjini Havana.

Msemaji wa Katibu amesema katika taarifa kuwa wawili hao wamekuwa na mazungumzo kuhusu masuala ya kimataifa ikiwemo Syria, Sudan Kusini, Jamhuri ya Afrika ya Kati na ile ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Halikadhalika wamejadili suala la uhakika wa chakulan na kuenea kwa silaha za nyuklia pamoja na malengo ya maendeleo ya milenia na mabadiliko ya tabianchi.