Ukatili dhidi ya wanawake ni ukiukwaji mkubwa zaidi wa haki duniani: Ban

Ukatili dhidi ya wanawake ni ukiukwaji mkubwa zaidi wa haki duniani: Ban

Ujumbe wetu uko bayana, wanawake na watoto wana haki ya kujisikia salama na kuishi maisha yenye utu mahali popote pale iwe kwenye mapigano, amani, umaskini au ustawi! Ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-

Moon katika kampeni ya UNiTE, iliyofanyika Havana Cuba, ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake.

Bwana Ban amesema ukatili huo hauwezi kumalizwa na serikali pekee bali juhudi za kila mtu zinatakiwa hata kwenye nchi kama Cuba..

 (Sauti ya Ban)

“Cuba iko mstari wa mbele kwenye mambo mengi ya maendeleo ikiwemo kupanua fursa kwa wanawake na wasichana. Imekabiliana na fikra potofu na kuweka taasisi za kusongesha usawa na kuzuia aina zote za ukatili. Hata hivyo kama ilivyo kwa nchi zote, bado kuna changamoto kwa ukatili dhidi ya wanawake na wasichana. Kutatua hali hii ni lazima tutambue kuna tatizo: Siyo kuficha wala kulipunguza.”

Katibu Mkuu amesema ni lazima kubadili mtazamo na tabia, sambamba na sheria na kuhakikisha zinatekelezwa na kusimamiwa huku akisema wanaume na wavulana wana wajibu muhimu kwani mara nyingi ukatili unaanzia kwa watu wa karibu wakiwemo baba, kaka, waume na hata wasimamizi.