Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wa WFP wa mchele na unga wa mahindi wawasili Bangui CAR

Msaada wa WFP wa mchele na unga wa mahindi wawasili Bangui CAR

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limesema Jumatatu malori yake yaliyosheheni msaada wa tani 250 za mchele na unga wa mahidi yamewasili mjini Bangui nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

 Malori hayo yamewasili baada ya safari ya kilometa 600 kutoka mpakani mwa Cameroon. Malori hayo ni sehemu ya msafara wa magari 60 uliosindikizwa na vikosi vya mpango wa kimataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya afrika ya Kati.

Msafara huo ulicheleweshwa na vizuizi vingi vya barabarani vilivyowekwa na makundi yenye silaha.