Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yataka wakimbizi wa Somalia wasilazimishwe kurejea makwao

UNHCR yataka wakimbizi wa Somalia wasilazimishwe kurejea makwao

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limetoa upya ombi la kutaka mataifa yanayohifadhi wakimbizi waSomaliakutowalazimisha kurejea makwao hususan maeneo ya kati nay ale ya kusini. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya

(Taarifa ya Grace Kaneiya)

UNHCR imesema ijapokuwa usalama umeikarika kwenye maeneo hayo ya kusini na kati ikiwemo mji mkuu waSomalia, Mogadishi, bado kuna mapigano na ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab.

Shirikahilolimesema mwaka jana wasomali 33,000 walirejea nyumbani lakini zaidi ya 43,000 walisaka hifadhi nchi jirani na kwingineko.

Msemaji wa UNHCR Fatoumata Lejeune Kaba amesema maelfu ya raia wanaendelea kupoteza makaziyaondani na nje yaSomaliaakiongeza kuwa wanawake wanakimbizi wako hatarini zaidi huku kukiwepo na ripoti za ubakaji bila watuhumiwa kuadhibiwa.

 “Mwongozo mpya wa UNHCR unasisitiza umuhimu wa serikali kutathmini maombi ya wasomali wanaotoka maeneo ya kusini na kati ya kusaka hifadhi ya kimataifa kwa misingi ya taarifa za uhakika za hali halisi huko Mogadishu na kwingineko. Taarifa inapasa kuzingatia athari za mapigano kwa raia. Raia wako hatarini kuuawa au kujeruhiwa kwenye mapigano kati ya jeshi la serikali na wanamgambo wa Alshabaab na hata katika mashambulio ya mabomu yanayowalenga. Hata Mogadishu, licha ya usaidizi wa jeshi la serikali kutoka kwa jeshi la Afrika, AMISOM bado AlShabaab wameendelea kuonyesha uwezo wao wa kushambulia.”

UNHCR inakadiria kuwepo kwa zaidiya wakimbizi Milioni Moja wa Somalia duniani kote.