Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji zaidi ya 45,000 walihatarisha maisha yao 2013 kuingia Italia na Malta:IOM

Wahamiaji zaidi ya 45,000 walihatarisha maisha yao 2013 kuingia Italia na Malta:IOM

Wakimbizi zaidi ya 45,000 walihatarisha maisha yao mwaka 2013 wakijaribu kuvuka bahari ya Mediteraniani ili kuingia Italia naMalta limesema shirika la kimataifa la uhamiaji IOM.

Idadi ya wahamiaji waliowasili ni kubwa zaidi tangu mwaka 2008, ukiacha mwaka 2011 ulioghubikwa na mgogoro waLibya. Kwa mujibu wa IOM wahamiaji zaidi ya 42,900 waliwasili Italia na wengine 2,800 waliingiaMalta.

Kwa wale walioingia Italia zaidi ya 5000 walikuwa ni wanaume na zaidi ya 8000 walikuwa ni watoto. Wengi wa wahamiaji hao waliingilia Lampedusa na wengine Syracuse Cicily.