Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misaada ya kibinadamu bado haijafika Homs:UM

Misaada ya kibinadamu bado haijafika Homs:UM

Mashirika ya misaada ya Umoja wa mataifa nchini Syria bado hayajapata ulinzi unaotakiwa ili kuwawezesha kufikisha misaada ya kibinadamu inayohitajika haraka kwa maelfu ya raia waliokwama kwenye mji wa Homs. Flora Nducha na maelezo kamili

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema liko tayari kupeleka mgao wa chakula kwa familia 500 na tani 500 za migfuko ya unga wa ngano ambnayo itatosheleza kulisha watu 2500 kwa mwezi mzima.

WFP pia itapeleka lishe maalumu ambayo itasaidiakamatiba kwa watoto waliodumaa na walio na utapia mlo uliokithiri . Mbali ya hayo ina chakula kilicho tayari kitakachogawiwa kwa kina mama na watoto ambao wataamu kuondolewa kutoka mji wa Homs pale patakapowezekana.

Elizabeth Byrs ni msemaji wa WFP mjiniGeneva.

“WFP inatetea upatikanaji wa fursa kwa maeneo yote ya Syria ambako fursa ya kuzifikia jamii kwa sasa ni ndogo. WFP na washirika wake wamekuwa na fursa ndogo kwa miji mingine Homs ikiwemo Al Rastan, Al Houlah, Talbisah, Ter Ma’ala na Ghanto, hii inamaanisha kwamba usambazaji wa chakula umewezekana tuu kila miezi 3 hadi 6 kwa kupitia misafara ya mashirika tofauti wakati hali ikiruhusu. WFP inazidi kuwa na hofu ya watu wanaoishi katika maeneo ambayo ni vigumu kuyafikia nchini humo wakikosa msaada wa chakula.Zaidi ya watu 775,000 mjini Al-Raqqa, Al-Hassakeh na Deir Ezzor hawajafikiwa na msaada wa WFP kwa miezi kadhaa  huku maeneo mengine zaidi ya 40 katika vitongoji vya Damascus bado vinazingirwa na hali hiyo inaathiri watu wapatao 800,000.”

Naye msemaji wa UNICEF Marixie Mercado anasema shirikahilopia liko tayari na madawa ya dharura na vifaa vua usafi.

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)

“UNICEF ina orodha ya vifaa vya kupeleka kwa idhini ya serikali. Orodha hii inajumuisha vifaa vya dharura vya madawa ,na vifaa vya kutibu kipindupindu, vinajumuisha sabuni, vitu vya usafi , dawa za kusafisha maji na maji yaliyochanganywa na chumvi, nguo za msimu wa baridi kwa watoto wachanga na chanjo ya polio.”

Fursa ya kufikisha misaada ya kibinadamuHomsni moja ya masuala yaliyojadiliwa katika mazungumzo ya amani yaSyriayanayoendeleaGeneva.  Jumapili serikali yaSyriailisema wanawake na watoto wako huru kuondoka mji uliozingirwa waHomshuku makundi yenye silaha yameahidi kuruhusu kupita kwa amani misafara ya misaada. Hata hivyo mashirika ya misaada yanasema hakikisho la usalama bado halijapatikana.