Wakulima wa nazi Ufilipino wako taabani baada ya kukumbwa na kimbunga

27 Januari 2014

Wakulima wa minazi nchini Ufilipino wapo katika mahitaji makubwa ya kurejesha kilimo cha zao hilo kilichoharibiwa na kimbunga Haiyan kilichoipiga nchi hiyo Novemba mwaka jana.

Kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo FAO, kimbunga hicho kilisababisha uharibifu mkubwa ikiwemo kuangushwa mamilioni ya miti ya minazi.

Inakadiriwa kuwa miti zaidi ya milioni 33 iliharibiwa na kimbunga hicho ni kikubwa kuwahi kulikumba taifa hilo.Mamlaka ya zao la nazi nchini humo imesema kuwa athari zilizosababishwa na kimbunga hicho inafikia dola za Marekani milioni 396.

Zao na nazi ni moja la zao linalotegemewasananchini Ufilipino. Taifa hilo ni la pili kwa uzalishaji wa nasi kwa wingi duniani.