Mtaalamu wa UM aitaka Qatar kutumia fursa iliyonayo kurekebisha mfumo wa sheria

27 Januari 2014

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa majaji na wanasheria, Gabriela Knaul ameisihi Qatar kutumia kile alichoita fursa ya kipekee kufanya marekebisho yenye lengo la kuimarisha mfumo wake wa sheria na haki ili kushughulikia changamoto inaozikabili. George Njogopa na ripoti kamili.

(Taarifa ya George)

Akiwa mwishoni mwa ziara yake ya siku nane Mjini Doha, mtaalamu huyo amesema kuwa Qatar inapaswa kuchukua jukumu la kuendesha mabadiliko katika vyombo vyake vya utoaji yake kwani ina kila sababu ya kufanya hivyo kutokana na kubarikiwa vyanzo vingi vya kimapato.

Amesema kuwa tofauti na mataifa mengi duniani, Qatar ina njia za kiichumi kufanikisha mageuzi hayo hivyo akaihimiza kuchukua hatua za haraka.

Kwa upande mwingine aliisifia Qatar namna ilivyopiga hatua tangu iliporidhia kwa mara ya kwanza sheria ya mahakama mnamo mwaka 2003, na mfumo wa Katiba mpya ya mwaka 2004.

Alisema kuwa kwa kutizama uhalisia wa mambo,Qatar imefanikuwa kuweka kile kinachojulikana “ mgawanyo wa madaraka” unazingatia na kujali uhuru wa mahakama lakini alisema kuwa kuna baadhi ya maeneo  maeneo machache yanapaswa kuzingatiwa .

Wakati wa ziara yake hiyo iliyoanza January 19 na kufikia kilele chake January 26 mtaalamu huyo alikutana na maafisa wa serikali, ikiwemo Waziri wa Sheria, Majaji na wanadiplomasia wanaziwakilisha nchi mbalimbali.