Ban ziarani Cuba, asema amani,usalama na maendeleo kumulikwa

27 Januari 2014

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon yuko ziarani nchini Cuba kuhudhuria mkutano wa jamii ya Amerika Kusini na mataifa ya Caribbean, CELAC.

Akizungumza muda mfupi baada ya kuwasili nchini humo Bwana Ban amezungumzia matarajio yake katika ziara hiyo ambayo pia inajumuisha kumbukumbu shujaa wa Cuba na Latin Amerika José Marti.

(SAUTI YA BAN)

"Natarajia kusikiliza maoni kuhusu masuala ya msingi ikiwamo usalama na amani pia maendeleo andelevu na haki za binadamu. Natarajia pia kukutana na maafisa wa Cuba akiwemo rais Raul Castro na mawaziri wengi. Tutajadili masuala mengi kuhusu maendeleo amani, usalama na mafanikio. Cuba inapitia kipindi muhimu cha mchakato wa mabadiliko nina shauku ya kujifunza na kuzungumza namna Umoja wa Mataifa unavyoweza kuendelea kusaidia katika mchakato huu."

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter