CAR imefikia katika hali mbaya saana, aonya Pillay

27 Januari 2014

Jamhuri ya Afrika ya Kati sasa imefikia katika hali mbaya saana ameonya Jumatatu Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa Navi Pillay , huku kukizuka upya mapigano na wapiganaji wa zamani wa Seleka na raia wa Kiislamu Kaskazini mwa nchi.

Tangu Januari 21 mapigano baiana ya wapinzani wa Balaka na wapiganaji wa zamani wa Seleka wanaoungwa mkono na raia wa Kiislamu wenye silaha katika vitongoji vya jirani na Bangui vya PK5, PK11, PK12 and PK13,yamesababisha vifo vingi.

Vikundi vimeingia katika uporaji maduka, nyumba na misikiti katika maeneo ya Waislamu vya vitongoji hivi. Cecile Poully ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu.

 (SAUTI YA CECILLE POUILLY)

Mapigano hayo pia yamewalizimisha wapiganaji wa zamani wa Seleka na raia wa Kiislamu kukimbilia mji wa Damara, uliopo kilometa 65 Kaskazini mwa Bangui.