Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mustakhbali wa amani ya Syria umeingia hatua muhimu Jumatatu

Mustakhbali wa amani ya Syria umeingia hatua muhimu Jumatatu

Mazungumzo ya amani ya Syria yanaendelea tena Jumatatu mjini Geneva ambapo serikali na wapinzani wanatarajiwa kuanza majadiliano kwa kuzingatia tamko la Juni 2012 ambalo linataka kuanzishwa kwa serikali ya mpito. Grace Kaneiya na taarifa zaidi

(TAARIFA YA GRACE KANEIYA)

Pande hizo mbili zimekuwa na mazungumzo ya ana kwa ana Jumamosi na Jumapili chini ya uwenyekiti wa mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa na muungano wan chi za Kiarabu Lakdhar Brahimi.

Mjadala wa mwishoni mwa wiki ulijikita katika upatikanaji  wa fursa za kibinadamu kwa mji wa Homs ulio chini ya machafuko kwa muda mrefu na pia kuachiliwa kwa mahabusu wanaoshikiliwa na serikali na majeshi ya upinzani.

Bwana Brahimi amesema hali nchiniSyriaimekuwa tata kwa muda na ni mapema mno kutabiri majadiliano yatadumu kwa muda gani.

(SAUTI YA BRAHIMI)

 “Haya ni majadiliano ya kisiasa. Kila kitu tunachojadili ni cha kisiasa. Katima siku ya kwanza hakuna mtu alitoa taarifa ya ufunguzi, ni mimi tuu.Natarajia pande hizi mbili kutoa tamko kuhusu njia ya kusonga mbele. Majadiliano yetu sio mahali pa kuu pa kujadili masuala ya kibinadamu. Lakini nadhani wote tumehisi na pande hizi mbili zihisi kwamba huwezi kuanza majadiliano kuhusu Syriabila kuwa na mjadala kuhusu hali mbaya saana ya kibinadamu iliyopo.

Umoja wa Mataifa unakadiria kwamba zaidi ya wait 100,000 wameuawa katika miaka mitatu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na watu milioni 9.5 wametawanywa ndani na nje ya nchi hiyo na wanahitaji msaada wa kibinadamu.