Skip to main content

IOM imepeleka msaada wa majira ya baridi kwa Wasyria walioko Uturuki:

IOM imepeleka msaada wa majira ya baridi kwa Wasyria walioko Uturuki:

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limepeleka misaada ya kibinadamu kwa ajili ya majira ya baridi kwa familia za wakimbizi wa Syria zaidi ya 3,160   kwenye mji wa  Kirikhan jimbo la  Hatay nchini Uturuki tangu wakati wa Krismasi ili kukabiliana na baridi kali na mazingira magumu wanayoishi.

Familia hizo zenye watu jumla ya 16,370 zimepokea mablanket zaidi ya 4,600, mito4800, magodoro 3450 na mazuria karibu 1100.  Mblanketi mengine 10,000 , mito 10,000 , vitanda 5000 na mazulia 2500 zitapewa familia zingine katika siku zijazo.

IOM pia imegawa majiko ya ya kupikia ya mafuta ya taa kwa familia 140, huku zingine 600 zikipokea majiko ya mkaa kwenye miji ya Hatay na Reyanli.

Mbali ya vifaa vya baridi IOM inatoa msaada wa fedha taslimu kwa kupitia vocha ambazo zitawasaidia kununua chakula na vifaa vya usafi. Mradi huo wa fedha unafadhiliwa na tume ya Muungano wa Ulaya ECHO na lengo ni kuwasaidia wakimbizi wa Syria wanaoishi Kirikhan mpakani mwa Syria na uturuki. Kuna jumla ya wakimbizi 25,000 wanaoishi katika eneohilona wengi wako katika hali mbaya.