Upatikanaji wa huduma ya maji safi waangaziwa nchini Tanzania

24 Januari 2014

Ikiwa ni miezi miwili kabla ya dunia kuadhimisha siku ya maji duniani, wataalamu wamekuwa wakibonga bongo juu ya nini kufanya ili huduma hiyo adhimu iweze kuwafikia wananchi wengi bila gharama kubwa. Mathalani kongamano la Zaragoza huko Hispania lilifanyika kama maandalizi ya siku hiyo likimulika maudhui ambayo ni umuhimu wa maji na nishati na uhusiano kati ya mambo hayo mawili.

Hapo wataalamu wakiwemo kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau walijadili changamoto, uhusiano na suluhisho la pamoja katika kuhakikisha upatikanajI wa uhakika na endelevu  wa maji na nishati. Maji na nishati vina umuhimu mkubwa katika ajenda ya maendeleo endelevu baada ya 2015.

Takwimu zinaonyesha kuwa kufikia mwaka 2015 watu Bilioni 50 duniani kote watahitaji maji na nishati huku kukiwa na mkwamo kuhusu fursa za upatikanaji wa huduma hizo na suala la matumizi yanayozingatia uhifadhi wa mazingira. Je barani Afrika hususan Tanzaniahali ikoje? Wilberd Kiwale wa radio washirika ORS FM ya Manyara nchini humo anaangazia sualahilo.

 (PCKG YA WILBERD)

Huo ni upande wa Tanzaniabara, je Tanzaniavisiwani hususan Unguja tuungane na Juma Ayoub wa radio washirika HITS FM kisiwani humo

 (PCKG YA JUMA)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter