Licha ya machafuko WFP inaendelea kutoa msaada CAR:

24 Januari 2014

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema linaendelea kutoa msaada wa chakula kwa wakimbizi wa ndani katika mji mkuu Bangui  na miji mingine ya Bouar na Bossangoa licha ya machafuko yanayoendelea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Shirika hilo limeongeza kuwa usalama mdogo umesababisha maelfu ya watu kushindwa kurejea makwao na pia kuingilia shughuli za usambazaji wa misaada ya kibinadamu.

WFP imetoa wito wa kuhakikisha barabara kuu za nchi hiyo zinakuwa na usalama ili kuruhusu wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu kupata fursa ya kutimiza wajibu wao.

Shirika hillimeongeza kuwa kutokana na matatizo barabarani malori 38 ya liyo na tani 1600 za chakula cha msaada wa WFP yamekwama kwenye mpaka wa Jamhuri ya Afrika ya Kati na Cameroon.

Chakula hicho kinaweza kulisha watu 155,000 kwa mwezi mmoja. Madereva wa malori hayo wamegoma kuingiaBanguikutokana na kutokuwepo usalama barabarani.