Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa ushirikiano wa nchi za Kusini kusaidia uhakika wa chakula Angola

Mradi wa ushirikiano wa nchi za Kusini kusaidia uhakika wa chakula Angola

Uhakika wa chakula nchiniAngolaambao umekuwa wa mashaka sasa umepatiwa shime kufuatia makubaliano ya mradi wa miaka miwili kati ya nchi hiyo naBrazilna ushirikiano wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO.

Mradi huo wa miaka miwili unagharimiwa kwa pamoja na nchi mbili hizo kwa thamani ya Dola Milioni Mbili nukta Mbili ukiwa ni ushirikiano kati ya nchi za Kusini ukihususha utafiti wa kilimo na mifugo.

Kupitia mradi huo wataalamu wa kilimo kutokaAngolawatapatiwa mafunzo ya muda mfupi ya kiufundi kwenye kituo cha utafiiti wa kilimo na ushirikiano cha Brazili, EMBRAPA, kituo ambacho kilikuwa na dhima kubwa katika mafanikio ya Brazili ya kupunguza njaa.

Mkurugenzi msaidizi wa FAO kuhusu ushirikiano wa kiufundi Laurent Thomas amesema kuwepo kwa watafiti na wagunduzi wenye sifa wanaoelewa changamoto za maendeleo ni jambo muhimu katika kuleta mapinduzi ya kilimo na uhakika wa chakula nchiniAngola.

Mradi huo utabuni mkakati wa kitaifa wa mapinduzi ya kilimo pamoja na kutoa mafunzo kwa jumla ya watafiti 105 kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo na ile ya utafiti wa mifugo nchiniAngola.

FAO ilianzisha ushirikiano wa nchi za kusini mwaka 1996kama njia mojawapo ya kurahisisha ushirikiano baina ya nchi hizo katika kuinua uhakika wa chakula.